Skip to content

Posts from the ‘Kiswahili’ Category

6
Jun

Dhana ya Msingi ya Indaba Endelevu

na Indaba Endelevu.

Lengo la Indaba Endelevu ni kutia nguvu kazi ya utume, mahali husika na ulimwengu mzima  kuwezesha  ushiriki kamili kati ya madayosisi ya ulimwengu wa kusini na kaskazini yakitumia vielelezo vipya ili kuunda dhana ya msingi. Dhana  hii imeweka msingi kazi yote ya Indaba Endelevu. Read more »

3
Jun

Mchakato wa Indaba

Kujenga na kukuza uhusiano katika kanisa lenye afya

  • Indaba huonyesha kibiblia  kipaumbele katika uhusiano:

Hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi na ushirika wetu ni pamoja na Baba na pamoja na Mwana wake Yesu Kriso.
1Yohana 1:3

  • Indaba huwezesha mazungumzo katika mambo muhimu:

kama ilivyokuwa karne ya kwanza, tunaweza kumtazamia Roho Mtakatifu  kutuhimiza kusikilizana sisi kwa sisi, kuelezeana  kwa wazi ufahamu mpya na kukubali maana mpya ya Injili kwetu, ikiwa kwa maumivu au kwa furaha.

Acc-3 1976

  •  Indaba inalenga kutia nguvu kazi ya Injili mahali husika na ulimwenguni pote:

Kielelezo cha Indaba pia kimewezesha utajiri zaidi wa muingiliano katika utume wa maridhiano unaoimarisha  uhusiano binafsi kati ya mtu na mtu na kati ya madayosisi mbalimbali, unaendeleza maelewana ya kina na mazungumzo ya pamoja na mahali ambapo  kumekuwa na tofauti katika  mambo tete na nyeti. Read more »

31
May

Dhima

Biblia inasema kuwa tumeitwa katika jamii kila mmoja kupitia uhusiano wetu na Yesu Kristo (1Yohana 1:3). Jamii ya watu wa Mungu  iliundwa kutoka kipindi cha utumwa na  Kutoka utumwani. Katika Agano Jipya tunasoma Yesu anaanzisha jamii yake kwa kuwachukua wafuasi wake katika safari ya huduma. Mtume Paulo hakufanya safari zake za uanzishaji wa makanisa tu bali aliyatembelea mara kwa mara na kuyaunganisha  pamoja kupitia wale alioandamana nao katika safari zake. Jamii ya Mtume Paulo ilipambana na tofauti zilizo jitokeza katikati yao ili kuwa sahihi au kupata usahihi wa mambo katika upelekaji wa  mawazo yao ambayo kwayo jamii inayo wazunguka inamawazo tofauti tofauti  juu ya huduma. Read more »