Skip to content

June 6, 2012

Dhana ya Msingi ya Indaba Endelevu

by Admin

na Indaba Endelevu.

Lengo la Indaba Endelevu ni kutia nguvu kazi ya utume, mahali husika na ulimwengu mzima  kuwezesha  ushiriki kamili kati ya madayosisi ya ulimwengu wa kusini na kaskazini yakitumia vielelezo vipya ili kuunda dhana ya msingi. Dhana  hii imeweka msingi kazi yote ya Indaba Endelevu.

Dhana ya Msingi.

  • Utume ni utume wa mahali  husika hufanyika mahali fulani na huwahusu watu na mahusiano miongoni mwao na kati yao na Mungu.
  • Utume wote ni wa ulimwengu wote. Utume wa kanisa katika eneo moja ni utume wa kanisa lote ulimwenguni.
  • Utume wa ulimwengu wote hauwezi kuwa utume wa mahali pengine isipokuwa una mizizi ya mazingira husika. Kwa hiyo kama kanisa fulani lingejiuliza kuhusu mchango wake ni nini katika utume wa ulimwengu; kimsingi ni utume wake katika mazingira yake kwa kushirikiana na kanisa la Kristo ulimwenguni.
  • Utume wa mahali husika utakuwa ‘wakujitenga , kujifungua na wenye mtazamo binafsi’ usipofahamu utume wa ulimwenguni pote

UFAFANUZI

Kuanzia mwanzo mwa harakati za utume wa sasa wapelekwa walikuwa ni wale waliokwenda kuhubiri Injiri katika nchi ya ugenini. Utume kilikuwa kitu kilichofanywa hasa na watu weupe, wanaume na wanawake toka ‘nchi za Kikristo’ kwenda kwenye nchi za kipagani kwa kawaida za Afrika na Asia. Baadaye utume ulihusisha ufadhiri wa miradi. Katika mambo yote mawili makanisa ya ulimwengu wa kaskazini yalitoa raslimali za ‘utume’ katika ulimwengu wa kusini.

Watu wengi bado wanafikiri yakuwa njia hii ndiyo utume wa ulimwenguni pote. Kama kanisa fulani huko Uingereza, Amerika ya Kaskazini au Australia likiulizwa linafanya nini katika utume wa ulimwenguni pote, litazungumzia msaada wa mradi wa maji huko Sudan, makazi ya yatima huko India au kutuma washirika wa kanisa lao huko Nepal. Haya yote ni mazuri, lakini wajibu halisi wa Kanisa lolote katika utume wa ulimwenguni pote ni katika mazingira yake mahali husika

Uelewa huu kwamba utume ni kile ambacho wenye nguvu wanafanya katika eneo jingine la kijiografia una msingi wa ukoloni. Wapagani waliambiwa maana ya Ukriso nayo ilikuwa jinsi ya kuvaa na kumkubali Yesu. Wapelekwa walishinikiza utamaduni wa muziki, majengo ya kanisa na elimu kuwa ndiyo alama muhimu za utume wa ‘Kikristo’

Askofu Zac Nyringie anatoa mwito kwa kanisa kuiga mfano wa Paulo kule Athene (Andrew Walls and Cathy Ross, eds, Mission in 21st Century, London, DLT,2008, 22-3). Paulo alisikiliza kabla ya kuhubiri na alitafsiri ujumbe wa Kristo katika mtazamo wa utamaduni wa mahali pale. Wajibu wa Mwinjilisti ni uleule hata leo. Kusikiliza na kutafsiri utume wa ulimwenguni pote usiojali mazingira ya mahali husika ni shinikizo la wenye nguvu. Kwa njia nyingine ni utume  wenye ‘kujitenga, kujifungia na kuwa na mtazamo binafsi’ (Andrew walls and Cathy Ross, eds, Mission in 21st Century, London, DLT, 2008, 22-3).

Utume wa mahali husika  utakosa maono na kutawaliwa na mambo madogo madogo, usipotambua nafasi yake katika utume wa Mungu wa ulimwenguni pote. Makanisa yanayokuwa, huwa yanaushirikiano na mengine sehemu mbalimbali ulimwenguni, wale wanaoshiriki mazungumzo ya awali wametiwa moyo kuutazama utume wao wa sehemu husika katika mtazamo wa ulimwenguni pote na pia kuona kuwa mahali walipotembelea utume unahusu mazingira husika.

Comments are closed.

%d bloggers like this: