Skip to content

June 3, 2012

Mchakato wa Indaba

by Admin

Kujenga na kukuza uhusiano katika kanisa lenye afya

  • Indaba huonyesha kibiblia  kipaumbele katika uhusiano:

Hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi na ushirika wetu ni pamoja na Baba na pamoja na Mwana wake Yesu Kriso.
1Yohana 1:3

  • Indaba huwezesha mazungumzo katika mambo muhimu:

kama ilivyokuwa karne ya kwanza, tunaweza kumtazamia Roho Mtakatifu  kutuhimiza kusikilizana sisi kwa sisi, kuelezeana  kwa wazi ufahamu mpya na kukubali maana mpya ya Injili kwetu, ikiwa kwa maumivu au kwa furaha.

Acc-3 1976

  •  Indaba inalenga kutia nguvu kazi ya Injili mahali husika na ulimwenguni pote:

Kielelezo cha Indaba pia kimewezesha utajiri zaidi wa muingiliano katika utume wa maridhiano unaoimarisha  uhusiano binafsi kati ya mtu na mtu na kati ya madayosisi mbalimbali, unaendeleza maelewana ya kina na mazungumzo ya pamoja na mahali ambapo  kumekuwa na tofauti katika  mambo tete na nyeti.

Taarifa ya tathmini ya Indaba Endelevu

 

Indaba ni safari

Biblia imejaa safari ambazo ni za wale walioamua kufuata  wito wa Mungu, wakiwa na ufahamu kidogo au pasipo ufahamu wa kule waendako. Ni katika safari hiyo ndipo tunajaribu kugundua kwa pamoja nia ya Kristo.

Kuamua kuanza

Uamuzi wa kuanza safari ya Indaba ni kujitoa kwa uaminifu kumfuata Kristo kwa pamoja katika mazingira husika. Indaba inaweza kufanyika ndani ya dayosisi au mtaani, kati ya madayosisi au vyuo vya theologia, kimataifa  au mahali husika. Kama ilivyo safari zote safari ya Indaba inahitaji maandalizi. Katika hatua ambayo jamii zipo tayari kuanza ndaba , hiyo nayo ni safari.

Nani anafanya Indaba?

Kuna wajibu mbalimbali katika Indaba, ni asili ya Indaba kwamba, washiriki wahusike katika kila hatua.

Viongozi –ni wale wanaowaalika watu katika mazungumzo na kuainisha mada muhimu.

Washiriki – ni wale wanaoishi kwa mujibu wa Indaba; wale wanaoanzisha mahusiano na kuingia katika mazungumzo rasmi; washiriki wawe na lengo la wazi na waumiliki mchakato.

Waandaaji – ni wale wanaowawezesha washiriki kwa kuendesha mpango kamili wakifanya kazi na muwezeshaji kwa kuwakutanisha watu na kuendesha mazungumzo rasmi.

Wawezeshaji – ni wale wanaotoka nje ya jamii ya Indaba kuongoza mchakato, kuwezesha mazungumzo ya faragha na kuwawezesha washiriki kufikia malengo waliyojiwekea wenyewe. Wawezeshaji ni ufunguo wa Indaba.

 

Safari ya Indaba

Hatua ya 1Kushirikisha Ono

viongozi wenye hamu ya kuwa na Indaba, watawashirikisha ono wote wanaohusika. Pande zote zinahitaji ushiriki katika kuandaa wazo la pamoja na safari ya Indaba. Viongozi wataandaa mada za jumla kuhusu Indaba husika, kujadiliana na jamii yao.

Hatua ya 2Mkusanyiko

Washiriki wanaalikwa kwenye safari ya Indaba. Wanaandaa pamoja ili waelewe lengo kwa wazi, wajitume na wahisi umiliki wa mchakato wa Indaba. Ni muhimu kuwaingiza kuanzia mwanzo wale ambao hawahusiki moja kwa moja ili umiliki wa mchakato uhusishe jamii kwa upana zaidi na pia katika kuombeana.

Hatua ya 3Kukutana

Lengo la kukutana ni kujenga uhusiano kwa njia ya safari ya pamoja ambayo kila mmoja anazamu ya kuwa mwenyeji na pia kuwa mgeni. Wote mwenyeji na mgeni wanagundua mtazamo wa kila mmoja na kila mmoja anagundua zaidi mtazamo wake ili kutafuta uhusiano wa kina na Kristo. Ibada na mtaala wa biblia ni muhimu sana vikundi vinapoendelea kujenga uhusiano kwa njia ya kugundua maisha yao ya kawaida katika mazingira yao kila mmoja. Shughuli zinahitaji kuchanganywa na muda maalumu wa kustarehe pamoja na kushiriki chakula cha pamoja.

Kutakuwa na shauku ya kutatua matatizo na sio ‘kupoteza muda’, lakini lengo ni kuanzisha uhusiano ambamo kila mshiriki atamtambua Kristo aliyomo kwa mwenzie.

Kunapokuwa na kuaminiana na uhusiano uliojengwa katika ufahamu halisi, kutakuwa na nafasi ya mazungumzo halisi.

Hatua ya 4Mazungumzo Halisi

Mazungumzo yaliyowezeshwa hutoa nafasi kwa washiriki kuwa wazi kuzungumza ukweli katika upendo na kuwa tayari kusikiliza ukweli unaozungumzwa kwao. Ni nafasi ya kujitoa muhanga ili kupokea changamoto ya hisia za ndani za mtu ili wote wageuzwe katika nia ya Kristo. Lengo ni kwamba mazungumzo yazae nguvu zaidi kwa ajili ya utume.

Hatua ya 5Kutoka Nje

Matunda ya Indaba ni ufahamu wa kina wa umoja wa Kanisa unaotokeza ushiriki wa pamoja katika utume wa Mungu.  Indaba inahitaji kuwasilishwa na wote wanaohusika ili jamii zao ziwezeshwe kutembea pamoja kama washirika katika utume wa Mungu.

Indaba endelevu inaweza kusaidiaje?

  • Kutoa vifaa vya kitheologia na vya kimchakato
  • Kutoa au kufundisha wawezeshaji
  • Kutoa ushauri uelekezi katika mipango
  • Kutoa fursa ya mdahalo kwa ajili ya kuchunguza mawazo na kusaidiana

Comments are closed.

%d bloggers like this: