Skip to content

May 31, 2012

Dhima

by Admin

Biblia inasema kuwa tumeitwa katika jamii kila mmoja kupitia uhusiano wetu na Yesu Kristo (1Yohana 1:3). Jamii ya watu wa Mungu  iliundwa kutoka kipindi cha utumwa na  Kutoka utumwani. Katika Agano Jipya tunasoma Yesu anaanzisha jamii yake kwa kuwachukua wafuasi wake katika safari ya huduma. Mtume Paulo hakufanya safari zake za uanzishaji wa makanisa tu bali aliyatembelea mara kwa mara na kuyaunganisha  pamoja kupitia wale alioandamana nao katika safari zake. Jamii ya Mtume Paulo ilipambana na tofauti zilizo jitokeza katikati yao ili kuwa sahihi au kupata usahihi wa mambo katika upelekaji wa  mawazo yao ambayo kwayo jamii inayo wazunguka inamawazo tofauti tofauti  juu ya huduma.

NJIA ZA MAJADILIANO ZILIIMARISHA MAHUSIANO KATIKA HUDUMA

Indaba’ ni neno la Kizulu linaloielezea mchakato wa jamii katika kutafakari masuala muhimu zaidi.  Michakato hiyo ni yakawaida katika jamii za Kiafrika, Asia, Visiwa vya Pasifiki na watu wa asili wa Amerika. Lengo kuu ni kuipa uhai na kuiendeleza zaidi jamii yao na si kutatua matatizo pekee.

Indaba Endelevu’ hutumia njia hii kuanzisha mahusiano na kuijenga jamii ili mazungumzo halisi juu ya mambo muhimu yaweza kuchochea utume.

Washiriki wa safari ya Indaba wanatiwa moyo kumwomba Mungu na kusoma Maandiko Matakatifu pamoja na kupokea mawazo ya wengine yatolewa katika katika mazingira yao; hivyo jamii itakuwa mahali salama ambamo kila mshiriki ataweza kuingia katika majadiliano yaliyowezeshwa. Hapa wanaweza kupambana  kwa tofauti zao kwa kusikilizana na muhimu zaidi  nikumsikiliza Mungu kwa pamoja bila kujali tofauti zao. Lengo ni kumsaidia kila mmoja kuwa na imani thabiti na kuwa mfuasi wa kweli wa Kristo; lakini pia kutafuta njia sahihi ya wote kushiriki katika kufikisha mawazo yao yenye kuboresha huduma.

Mfumo huu ulianzishwa kwa kushauriana na wanatheologia kutoka Afrika, Asia, Amerika ya Kaskazini, uhindi magharibi na Uingereza.  Walikutana katika makundi tisa wakitafakari Maandiko na michakato ya namna ya utatuzi wa maswala mbalimbali kufuana na tamaduni zao. Baada ya majadiriano marefu waliandaa maandiko ambayo ni muongozo wa kuisimamia na kuiendeleza  Indaba Endelevu .

Matokeo ya mchakato yalijaribiwa na kufanyiwa masahihisho katika vikao Vinne Vya Mazungumzo ya Majaribio, kikao kimoja katika kila Dayosisi kati ya madayosisi matatu.

Tathmini ya Mazungumzo ya majaribio ilionyesha kuwa mtindo wa Indaba na uzoefu uliyopatikana unafaa kwa sababu unaimarisha maelewana na kusaidia utume kwa njia ya upendo.

Askofu Paul Kwong- Askofu Mkuu wa Hong Cheng Kung Hui anasema:-

Indaba pia inahamasisha majadiliano mapya juu ya mambo mbalimbali yahusuyo huduma kutoka pande zote, lengo ni kutafuta ukweli halisi wa mambo wenye kuaminika na kupata njia za kisasa za usuluhishi ambazo si za kuegemea mawazo fulani tu yasiyo badilika ndani ya jamii yenye mawazo na fikra tofauti. Lakini kuhamasisha mawazo zaidi na kusikilizana na utayari wa kuchambua kwa kina kwa lengo la kushirikishana mambo ya muhimu yanayo patikana katika msingi au mizizi ya imani yetu.’

Maelezo ya Msingi

Mwaka 1996 mkutano wa Maaskofu Wakuu uliofanyika katika mji wa Alexandria ulikubali taarifa ya The Windsor Continuation Group iliyosema :-

‘Tunahitaji kutoka katika mfumo wa kutokukubali mabadiliko yatokanayo na mawazo au fikra mpya ambazo ni tofauti na mawazo halisi ya mwanzo hivyo kuzuia mawazo mengine yanayo jadili juu ya habari za Mungu’

Kuna jambo la muhimu lililozoeleka kuhusu njia mbalimbali zitumikazo na kanisa la Kianglikana duniani katika utayari wa kukubali mawazo mbalimbali ambayo Wakristo wangependa kufahamu juu ya kweli ya Mungu kwa kujifunza kutoka kwa mawzo ya wengine na kulifanya kanisa lote kufahamu ukweli wote juu ya Mungu.

Kwa kujibu hilo Indaba Endelevu  imeanzisha  mtindo wa mazungumzo unaoweza kuitwa ‘kumsubiri Mungu kwa pamoja’ katika jumuia ya Kianglikana kwa kuendeleza mahusiano ambayo yataweka uwazi au mwanya wa majadiliano yenye kuwezesha kanisa lote kufahamu ukweli wote.

Jumuia ya Kianglikana inapenda kumshukuru Mch. Marta Weeks aliye tuamini sisi kutumia mchango wake wa kuendeleza mpango huu wa kuruhusu majadiliano na kukubaliana mambo yote ambayo msingi wake ni Maandiko Matakatifu na kutambua mawazo ambayo yanazingatia  tamaduni husika kwa vigezo au mawazo thabiti kwa lengo la kuimalisha huduma utumie duniani kote.

Pia tunatumia fursa hii kuishukuru Satcher Health Learning Institute (SHLI) kutoka Morehouse School of Medicine ambao wamesimamia upatikanaji wa fedha zisizo na mashariti.

Si hao tu lakini tunatumia fursa hii kuwashukuru Dayosisi ya Toronto na Hong Kong Sheng Kung Hui kwa mchango wao uliotusaidia kupiga hatua katika swala hili.

Comments are closed.

%d bloggers like this: